Wednesday, November 04, 2009

Mikakati


Waheshimiwawabunge wakipanga mikakati: Kutoka kulia ni Juma Kapuya (waziri wa kazi), Rostam Aziz (Igunga), Emmanuel Nchimbi (Naibu Waziri wa Ulinzi) na Andrew Chenge (Bariadi Magharibi)

Monday, November 02, 2009

Mbunge Sigfrid Ng'itu Afariki Dunia

Mbunge SIGIFRID SELEMAN NG'ITU,wa RUANGWA-CCM,LINDI, amefariki dunia. Kikao cha Bunge kimeahirishwa hadi kesho kutokana na msiba huo.

Mbunge huyo alikuwa amelazwa katika Taasisi ya Mifupa muhimbili (MOI) kutokana ugonjwa wa kiharusi, uliosababisha damu kuvilia kichwani, hivyo kufanyiwa upasuaji kutokana na tatizo hilo.

Spika wa Bunge, Samuel Sitta alisema jana kabla hajaahirisha bunge kuwa mbunge huyo pia alikuwa anasumbuliwa na tatizo la sukari na alipata malaria. Kamati ya bunge ya Utawala imekutana asubuhi hii kupanga taratibu za mazishi.

Tuesday, October 27, 2009

Lowassa Kukabwa Koo

Urafiki wa Lowassa, JK usiingilie urais-Wabunge

*Selelii, Kimaro wataka afikishwe kortini
*Walaumu serikali kwa kutoa majibu ya ovyo
*Lowassa: Sizungumzi na vyombo vya habari



WAKATI mkutano wa bunge unaanza leo, mzimu wa mkataba tata wa Richmond umeendelea kumwandama aliyekuwa Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa baada ya baadhi ya wabunge kudai kuwa anastahili kuchukuliwa hatua zaidi ya ile ya kujiuzulu kutokana na kutajwa kwake katika kashfa hiyo.

Wabunge hao kwa nyakati tofauti wamesema kuwa urafiki ambao Bw. Lowassa alisema upo baina yake na Rais Jakaya Kikiwete usiingilie urais, serikali na uiachwe ifanye kazi yake kwa kumchukulia hatua kutokana na kuliingizia taifa hasara.
Endelea nayo

Monday, October 26, 2009

Lowassa alivyoshiriki Richmond


Nyaraka zaonyesha kila hatua aliweka mikono yake

*Uthibitisho wa kuibeba Richmond watolewa peupe
*Kumbe ndiye aliipora Tanesco kazi ya kusaka mzabuni
*Wizara ya Nishari na Madini ilisubiri maamuzi yake .
*Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.

Kilio cha Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa (pichani), bungeni kwamba alidhalilishwa sana kwa kuhusishwa na mkataba tata wa kampuni ya Richmond, si lolote wala chochote baada ya uchunguzi wa kina wa nyaraka uliofanywa na gazeti hili kubaini kwamba alihusika vilivyo katika mchakato mzima wa zabuni hiyo. Source NIPASHE

Wednesday, October 07, 2009

Tovuti Buuuuuuuuuureeeeeeee!

JIPATIE TOVUTI BURE KABISA

Pole na kazi ya kuelimisha na kuburudisha jamii yetu.
Tumekuja na huduma mpya ya BURE kwa watanzania tu tunaomba uwafahamishe. Kuzingatia umuhimu wa kuwa na tovuti, na ya kwamba ni gharama sana hapa TZ kupata tovuti, na tena watu wanafanya biashara rasmi kwa barua pepe za bure kama yahuu na giimeili, hii yote inaonesha ukosefu au gharama kubwa ya kupata tovuti.

Sisi tumedhamiria kubadili uelekeo mzima wa upepo, na tumepata wasamaria wema na sasa rasmi tumefanikiwa kuleta ufumbuzi na neema kwa waTZ kwa suala la tovuti na anuani rasmi za barua pepe.

Na sasa kwa awamu ya kwanza kwa kuanzia tu, WATU 100 WATATENGENEZEWA TOVUTI BURE. Watu 100 kwa maana ya mtu binafsi, kampuni, biashara, shirika, asasi zisizochukua faida (NGO), kikundi, duka, mjasiriamali, saluni, shule ama Saccos n.k. BASI KILA ALIYEDHAMIRIA KUWA NA WEBSITE/TOVUTI ajiunge na utaratibu huu wetu atengenezewe TOVUTI MOJA BURE
KABISA.

TOVUTI HII YA BURE itamfanya mhusika aweze kupata anuani rasmi za barua pepe, yaani kama yeye ni Mwanahawa wa Vinyago Suppliers anatengenezewa anuani zake za barua pepe mfano mwanahawa@vinyagosuppliers.co.tz n.k kadiri ya atakavyo, nyingi apendavyo. Ataimiliki tovuti na kuiendesha yeye.

Kumbuka kwa awamu hii ya kwanza TUNATOA BURE TOVUTI 100 TU kisha awamu ya pili tutatangaza tena. Hebu fikiria kwa mkupuo tukipata tovuti 100 kwa maana ya kwamba tunakuwa na kurasa mia moja zinazoelezea watu/kampuni/vikundi mbalimbali na shughuli zao hapa Tanzania, hii ni hatua kubwa sana na inaongeza maingizo ya utafutaji wa vitu toka Tanzania katika search engines na tunasogea mbele taratiibu.

Hakuna vigezo vya kupata huduma hii ya bure, na tutahudumia kwa mujibu wa
FIFO (first in first serve/out) wa kwanza kuja, wakwanza kutoka/kuhudumiwa. Maelezo na ufafanuzi zaidi tafadhali tembelea http://www.tovutiyangu.com ujisomee huduma hii kwa undani. Zipo pia huduma na bidhaa mbalimbali kwa walio na tovuti tayari.

Ahsante sana.
Admin,
tovutibure (at) tovutiyangu.com
http://www.tovutiyangu.com

Saturday, August 29, 2009

Waraka: Waislamu Hatudanganyiki


Yamo mambo mengi ndani yake. Walioweza wamechambua haya

Wednesday, August 26, 2009

Sababu za Zitto kumpinga Mbowe

Naibu katibu mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe amesema ana sababu za msingi za kuamua kuuwania uenyekiti wa chama hicho, huku mwenyekiti wake Freeman Mbowe akimkaribisha katika kinyang'anyiro hicho.
Tumefukuza sana wanachama. Haiwezekani tukajenga chama cha kufukuzana tu. Ni lazima tukubali kutokubaliana," alisema.
"Kugombea kwangu ni wito wa kurejesha umoja katika chama wakati tunajiandaa kuchukua dola. Uchaguzi Mkuu wa 2010 utakuwa wa kihistoria kwa kuwa kwa uzoefu wangu unaweza kulazimisha serikali kuundwa na waziri mkuu ambaye hatoki CCM. Hatuwezi kwenda huko tukiwa divided (tumegawanyika)."
Soma kwa kina

Tuesday, August 25, 2009

Zitto Kumvaa Mbowe

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zitto Kabwe ameamua kushindana na mwenyekiti wake, Freeman Mbowe kwenye uchaguzi mkuu wa chama hicho mapema mwezi ujao. Zitto ambaye pia ni mbunge wa Kigoma Kaskazini tayari amerejesha fomu yake, na inasemekana amesema anataka kushindana na Mbowe ili kukiendelea chama, baada ya uwezo wa mwenyekiti kuishia hapo kilipo.

Mshahara wa Spika, Jaji Mkuu maradufu

Serikali imewaongezea mishahara viongozi wa kisiasa, majaji, wakuu wa mikoa na wilaya kuanzia Julai mwaka huu, huku jaji mkuu na spika wakiongezewa maradufu.
Habari za uhakika zilizolifikia gazeti hili zimeeleza kuwa mshahara wa jaji mkuu na spika, ambao ni viongozi wa mihimili mikuu miwili ya nchi, umepanda kutoka Sh2,760,000 hadi Sh4,850,000 kuanzia Julai na ongezeko hilo ni sawa na asilimia 75.7 Soma zaidi hapa

Kishindo cha Sitta Urambo

Mkewe, Margaret Akilakiwa na mashabiki

maandamo yaliyompokea kuingia Urambo

Mzee mwenyewe akilakiwa (kulia)


Hapa akihutubia tamasha la kwaya



Akisalimiana na wakazi wa kijiji cha Ndorobo waliomsimamisha ili kumsalimia na kumpa pole kwa yaliyomkuta huko Dodoma




Tuesday, August 18, 2009

Zombe huru, machozi yatawala

NDUGU wa wafanyabiashara watatu wa madini kutoka Mahenge mkoani Morogoro na dereva teksi wa jijini Dar es Salaam, waliouawa Januari 14 mwaka 2006 kwa tuhuma za ujambazi, jana walibubujikwa machozi baada ya Mahakama Kuu kuwaachia watuhumiwa wote wa mauaji hayo.
Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Salum Massati amemwachia huru aliyekuwa mkuu wa upelelezi mkoani Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Abdalla Zombe na askari wenzake nane waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya mauaji hayo ya kukusudia, akieleza kuwa ushahidi haukujitosheleza kuwatia hatiani.
habari ndiyo hiyo. Mtiririko mzima wa kesi hiyo ulikuwa hivi. Watu wanaionaje kesi hiyo? Msomi wa sheria anaelezea: Sheria ndivyo ilivyo.

Maoni ya Msomi: Kilichotokea ni sawa na alichowahi kusema mwanafalsafa mmoja, Swift Jonathan (1667 - 1745) kwamba "Laws are like cobwebs, which may catch small flies but let wasps and hornets break through" --Damian Gabagambi kupitia Bidii

Monday, August 17, 2009

Macho Yote Kwa Zombe

KIla inaposomwa taarifa ya habari, watu wanaacha kazi zote, wanafuatilia hukumu ya Kesi ya Zombe, Majibu yote yatapatikana hapa leo hii.

Thursday, August 13, 2009

Nyumbani ni Nyumbani


Monday, August 10, 2009

Mahanga Katika Mjadala wa Ufisadi

Kadri siku zinavyosogea, tunazidi kujipambanua kujua nani ni nani katika mjadala wa ufisadi. Mtu wa karibuni kabisa ni Mbunge wa Ukonga, Naibu Waziri wa Kazi,
Ajira na Vijana, Dk Makongoro Mahanga aliyekaririwa na Gazeti la Mwananchi Jumalipi akisema:
CCM kuna Mafisadi wanne tu; akimaanisha kuwa si wengi, hivyo hawastahili kiwango cha kelele kinachopigwa dhidi ya ufisadi. Na kuwa kelele hizo 'zinakichafua' chama chao. Leo mjumbe huyo wa NEC katoa taarifa mpya ya kufafanua alichosema jana: Isome kama ilivyotolewa: hapo chini:

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

KAULI YANGU KUHUSU SUALA LA UFISADI NDANI YA CCM
Katika ukurasa wa mbele wa gazeti la Mwananchi Jumapili toleo Na. 03345 la tarehe 09 Agosti 2009, kulikuwa na habari yenye kichwa cha habari “Mahanga: Mafisadi CCM ni wanne tu”. Habari hii inaeleza na kunukuu mazungumzo yangu na gazeti hilo kuhusu maoni yangu kuhusu mjadala unaoendelea ndani na nje ya Bunge kuhusu suala la ufisadi ndani ya CCM.

Nimesikitishwa na namna mahojiano yangu na gazeti hilo yalivyopewa kichwa cha habari cha kupotosha kabisa. Kichwa cha habari “Mahanga: Mafisadi CCM ni wanne tu” kinapotosha kabisa, siyo tu yale niliyoyasema, lakini pia hakiendani hata na habari yenyewe ilivyoelezwa kwenye gazeti hilo ukisoma habari hiyo nzima.

Kwa mfano, wakati kichwa cha habari kinataka wasomaji waamini kwamba nilisema “…. Kuna mafisadi wane tu CCM’, ukisoma ndani ya habari hiyo inaeleza kwamba nilisema “..Hawa wanaoitwa mafisadi wako wapi? Mbona hawatajwi?...” ‘Tathmini yake inaonyesha kuwa kelele zote za ufisadi zinawalenga watu ambao hawazidi wanne ndani ya chama hicho (CCM), na kwamba miongoni mwao, tayari wameanza kushughulikiwa’. Ni wazi kwamba hata hiyo nukuu ya hapo juu ina tofauti kubwa sana kimantinki na ki-ukweli na kichwa cha habari hiyo kama ilivyowekwa na gazeti hilo.

Huku nikipinga vikali kwamba sikusema hayo yaliyotolewa kwenye nukuu ya kichwa cha habari cha gazeti hilo, ningependa kuweka sawa yale niliyoyasema nilipopigiwa simu na mwandishi wa gazeti la Mwananchi Jumapili, Bw. Leon Bahati, ili kupata maoni yangu kuhusu mjadala huo na nilipoongea na mhariri wa gazeti hilo aliponipigia simu tena baadaye. Aidha napenda kuongezea maoni yangu ya ziada kuhusu suala hilo.

Nilichowaambia waandishi hao kama ilivyoelezwa kwa usahihi kwa asilimia kubwa ndani ya habari yenyewe ni kwambva wabunge na watu wengine ndani ya CCM wanaotamba kupambana na ufisadi na kutoa tuhuma nzito kwamba kuna mafisadi ndani ya chama wanaohatarisha uhai na ushindi wa CCM katika chaguzi zijazo, wanapambana na mafisadi hewa au wa kufikirika kwa kuwa wameshindwa kuwataja hao mafisadi waziwazi au kupeleka ushahidi wao kwenye vyombo vya dola kama TAKUKURU, Mahakama ama kwa Rais.

Nilisema kinachohatarisha ushindi wa CCM siyo hao “mafisadi” wa kufikirika au wa kubuni ndani ya CCM kama hao “wapambanaji” wanavyodai, bali ni kauli hizo za “wapambanaji” ndizo zitakiharibia chama kwani wananchi wasioelewa malengo yao halisi wanaweza kuamini kwamba kweli chama hiki kimejaa mafisadi na kukinyima kura.

Nikasema naamini hii ndiyo nia ya watu hawa wanaojiita wapambanaji wa ufisadi. Kwamba kwa makusudi tu ama kwa wivu na chuki zao za kisiasa wameamua kukiharibia chama chao ili wananchi wasione na kufurahia mambo mazuri na makubwa ya maendeleo yaliyotekelezwa na Serikali ya awamu ya nne ya CCM kwenye sekta za elimu, barabara, afya, maji, kuondoa umasikini na hata hilo la kupambana na rushwa na maovu mengine kwenye jamii, na badala yake wakihukumu chama kwa ufisadi wa kufikirika na uliotiwa chumvi unaoenezwa na hawa “wapambanaji”.

Ni kweli kabisa kwamba rushwa na ubadhirifu wa mali na rasilimali za umma ni mambo mabaya yanayorudisha nyuma maendeleo ya nchi yetu, na ni lazima wananchi wote tupambane nayo; na lazima tupongeze juhudi za Rais Kikwete na vyombo alivyoviunda na kuviboresha kama TAKUKURU na Mahakama katika kupambana na maovu hayo, na kama wananchi, ni budi tutoe ushirikiano kwa Rais na vyombo hivi katika mapambano haya, lakini watu wasiofuata utaratibu wa kutoa vielelezo na ushahidi kwenye vyombo husika na kubaki kutoa tuhuma za jumla jumla tu kwenye vyombo vya habari na majukwaa ya kisiasa hawasaidii nchi katika mapambano dhidi ya ufisadi, badala yake wanakuza chuki tu miongoni mwa jamii.

Lakini kibaya zaidi kama hao wanaotoa tuhuma hizo za kufikirika ni viongozi na makada wa CCM na wanatuhumu viongozi na makada wenzao ndani ya CCM bila kutoa ushahidi tena kwenye vyombo vya habari na majukwaa ya kisiasa bila kufuata taratibu za chama za kukosoana na kukemeana ndani ya vikao rasmi vya chama, basi wanakiharibia chama na kusaidia upinzani, na nikasema watu hawa kimsingi si “wenzetu” tena, bali ni wapinzani na ni vyema wakaondoka mapema kwenye chama hiki na kujiunga rasmi na upinzani, kwani wapinzani kushutumu CCM waziwazi ni mbinu za kawaida za siasa za upinzanani duniani.Lakini niliendelea kusema kwamba CCM, kama chama, siyo fisadi.

Inawezekana kuna wanachama wachache wasio waaminifu na wenye maadili mabovu na wala rushwa, lakini hao tuwashughulikie kwa taratibu za kutoa ushahidi na kufuata misingi ya sheria za nchi kama ambavyo watuhumiwa kadhaa walivyokwisha pelekwa mahakamani ambapo kesi zao zinaendelea kisheria.

Hata hivyo nilielezea gazeti hilo kwamba ingawa hawa “wapambanaji” wa ufisadi hawawataji wana CCM wenzao wanaowatuhumu kwa ufisadi, tathmini yangu ya kimazingira inaonyesha kwamba wanawanyooshea zaidi vidole watu wachache tu pengine wasiozidi wanne, siyo kwa kuwa wana ushahidi wa wazi wa ufisadi wao, lakini kwa maoni yangu, ni chuki na wivu tu wa kisiasa dhidi ya watu hao na kutaka watanzania wote warithi chuki na wivu wao dhidi ya watu hao.

Kwa tathmini yangu, sababu ya chuki na wivu huo unatokana zaidi na matokeo ya chaguzi za kitaifa zilizopita na zijazo, ambapo “wapambanaji” katika chaguzi zilizopita walikosa nafasi walizotaka za uongozi na madaraka nchini, na hivyo kujenga chuki dhidi ya hao wanaowaona kuwa ndiyo “king makers”, na kihistoria “king makers” duniani huwa hawapendwi na watu wengi.

Na ndiyo maana nikasema, hivi hata kama leo nchi hii ikaamua kwamba hawa wanasiasa wachache “mafisadi wa kufikirika” watoswe baharini au wafungwe maisha, je, CCM sasa itapona, au ndiyo itakuwa mwisho wa vitendo vya rushwa na ubadhirifu nchini mwetu? Mimi nasema hapana.

Mimi siwezi kumtetea mtu yeyote fisadi mradi ushahidi uanikwe wazi kwa kufuata mkondo wa sheria, lakini nisichokubaliana nacho ni kelele tu za ufisadi wa kufikirika na usiotolewa ushahidi thabiti kwenye vyombo vya sheria.

Nisichopenda ni tabia ya viongozi wa CCM kutofuata misingi ya chama ya kujadili mambo ya ndani ya chama na kukosoana kwenye vikao vya ndani ya chama. Sipendi wanandoa kugombana hadharani hadi kuvuana nguo na kuanza kufukuzana wakiwa uchi mitaani mbele ya watoto wao na watu wengine wa mitaani!

Kuhusu tuhuma zingine za kufikirika za “mafisadi” kupeleka fedha nyingi kwenye majimbo ya “wapambanaji wa ufisadi” ili kuwang’oa ubunge, nilisema kama ushahidi hauwezi kutolewa kuonyesha nani katoa fedha, kampa nani, lini, na zimepelekwaje kwenye majimbo hayo, basi shutuma hizi nazo ni za kufikirika, zisizokuwa na ukweli na ni woga tu wa hao wanaozitoa katika kujaribu kukandamiza demokrasia ya wagombea wengine kwenye majimbo hayo ili kupata huruma isiyostahili ya wapiga kura. Wengi kati ya hawa wanaopiga kelele hizo waliingia Bungeni mwaka 2005 baada ya kuwatoa wabunge waliokuwepo.

Je, wao “wapambanaji” walitumwa na mafisadi gani wakati huo ili kuwatoa waliokuwepo? Kama wameshindwa kuwashawishi wapiga kura wao kwa kutekeleza na kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kuondoa kero za wananchi wao, wasitafute wachawi.

Ni lazima sasa chama kisimame imara, kiache tabia ya kuogopa kuambizana ukweli na kiwakemee watu hao wanaotaka kukigawa na kukisambaratisha chama chetu, na ikibidi kiwavue uanachama ili tubaki na wanachama wanaokipenda chama chao kikweli na wanaofuata miiko, taratibu na maadili ya chama.

Dr. Milton Makongoro Mahanga, Mb, MNEC

Wednesday, July 29, 2009

Ana Kwa Ana na Spika


Kisima Cha Fikra (aliyeshika kifuani) akisalimiana na Mheshimiwa Spika Samuel Sitta katika viwanja vya Bunge, alipotembelea taasisi hiyo juzi na jana. Wengine wanaoangalia ni Mzee wa Mshitu (kati) na kushoto kabisa ni Bakari Machumu, Mhariri Mtendaji wa The Citizen. (picha na Jube Tranquilino) (picha zaidi tazama album)
KITABU CHA WAGENI Site Meter